Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka kwa kusema kuwa kwasasa hana mpango wa kuingia kwenye mahusiano na wanaume aliowazidi umri.

Shilole ambaye pia ni muigizaji wa Bongo Movie amesema kuwa kwa sasa yeye hana mahusiano na wanaume ambao amewazidi umri, kwani mpenzi wake wa sasa ni mwanaume halisi na amemfanya awe na mawazo ya kuwa mke.

Shilole amesema kuwa “Mwanaume wangu wa sasa sio serengeti boy, ni gentle man, anajielewa na pia ni mtu mzima, ananifanya mpaka nifikirie kuolewa niwe mke, yaani sio serengeti boy kabisa, na pia hataki kabisa mambo ya mitandao na ndio maana simuweki wazi.

Mwanamuziki huyo amewatetea watu ambao wana mahusiano na wanaume wanaowazidi umri na kusema siyo kitu cha ajabu kwani umri ni namba tu, kinachomata ni mapenzi.

Shilole alishawahi kukumbwa na sakata la kuwa na mahusiano na wanaume wenye umri mdogo (serengeti boys) akiwemo aliyekuwa mpenzi wake Nuhu Mziwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *