Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepokea Jumla ya Kompyuta za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo cha NIDA Textile Ltd.

Wakati wa kupokea kompyuta hizo Makonda amesema kuwa atazigawa kompyuta kwenye vituo vya Polisi 20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System).

Makonda amesema kuwa mfumo huo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu.

Makonda ameongeza kwa kusema kuwa taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa, Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA, Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitihada za mkuu huyo wa mkoa katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *