Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa atahakikisha ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za walimu pamoja na vyoo kwa shule za msingi na sekondari zitakamilika siku zijazo.

Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na sehemu ya chumba cha mwalimu Mkuu,Chumba cha Muhasibu, Chumba cha Katibu Muktasi pamoja na ofisi za Msaidizi wa Mwalimmu mkuu na walimu wote huku zikiwa na Vyoo vya kisasa pamoja na Bafu.

Makonda ameviomba vyombo vya Ulinzi na usalama vya Mkoa wa Dar es Salaam kumpatia mafundi wa ujenzi kama sehemu ya kuunga mkono jitiada alizoanzisha za ujenzi wa Ofisi hizo ambapo vyombo hivyo vimeridhia kumuunga mkono.

Ujenzi wa Ofisi hizo unategemea zaidi jitiada za wadau wa maendeleo ikiwemo wamiliki wa kampuni pamoja na Wananchi wenye dhamira ya kuona Walimu wanafanya kazi katika mazingira Mazuri.

Makonda amesema kuwa jitihada zake zimeanza kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kupata Mabati 11,000 na mifuko ya Saruji 1,000 ambapo Mahitaji ni Mabati 50,000, Mbao zaidi ya Million mbili  pamoja na vifaa vingine vya ujenzi.

Makonda amesema ataanza kutembelea viwanda vinavyojihusisha na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemoMabati, Saruji, Nondo na vinginevyo kuona namna wanavyoweza kuunga mkono ujenzi huo ili kuhakikisha walimu wanafanya katika mazingira rafiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *