Kesi inayomkabili Wema Sepetu imeendelea leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaamam.

Kesi hiyo ya matumizi ya bangi irihairishwa kusikilizwa kwa muda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kutokana na wakili anayemtetea Wema kutokuwepo mahakamani hapo.

Wema aliyefika mahakamani hapo akiwa ameambatana na mama yake mzazi, Mariam Sepetu na watuhumiwa wenzake, alichoieleza mahakama kuwa wakili wake ameshindwa kufika kwa wakati kutokana na majukumu mengine kwani anasikikiza kesi nyingine inayoendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Thomas Simba alipotaka kuiahirisha hadi siku nyingine, wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa anaomba kesi hiyo isikilizwe leo kutokana na shahidi upande wa serikali ambaye ni mkemia kuwepo kwa siku ya leo na kuanzia kesho anatarajia kusafiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *