Manchester United wamekamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kutoka Chelsea kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 40 baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Matic, 28, amekuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na United majira haya ya joto baada ya beki Victor Lindelof kwa ada ya paundi milioni 31 kutoka Benfica na Romelu Lukaku paundi milioni 75 kutoka Everton.
Baada ya kukamilisha usajili huo, Matic amesema ana furaha sana kujiunga na Manchester United wakati huu wa kutokana na ubora wa timu hiyo.
Mourinho, alipokuwa Chelsea, alitumia £21m kumnunua Matic kutoka Benfica kwa kipindi cha pili Stamford Bridge Januari 2014.
Thamani yake ilikuwa imekadiriwa kuwa chini ya £5m alipoihama klabu hiyo kama kikolezo wakati wa ununuzi wa David Luiz Januari 2011, miaka miwili baada yake kujiunga na Blues kwa mara ya kwanza kwa £1.5m kutoka kwa klabu ya MFK Kosice ya Slovakia.
Matic ameunga bao moja katika mechi 35 alizochezea Chelsea Ligi ya Premia msimu wa 2016-17, ambapo pia alifunga bao la kipekee wakati wa ushindi wao nusu fainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham Aprili mwaka huu.