Polisi nchini Malawi wametoa kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani Joyce Banda kuhusiana na sakata ya ulaji rushwa inayofahamika sana kama Cashgate wakati wa utawala wake.
Polisi wamesema wamepata ushahidi wa kuaminika kuhusiana na sakata hiyo ya $250m (£190m).
Kashfa hiyo, inaibua uwezekano kwamba huenda rais huyo wa zamani alitenda makosa yanayohusiana na kutumia vibaya mamlaka na utakatishaji wa fedha.”
Banda yuko nje ya nchi na polisi wan chi hiyo wamesema wataomba msaada kutoka kwa polisi wa kimataifa Interpol kuhakikisha anarejea nchini humo kujibu mashtaka.
Cashgate ndiyo sakata kubwa zaidi ya ufisadi kuwahi kutokea katika historia ya Malawi ambapo sakata hilo inahusisha kuporwa kwa fedha za umma wakati wa utawala wa Bi Banda.
Rais huyo wa zamani hajazungumzia tuhuma hizo zilizotolewa dhidi yake kuhusika katika kuhujumu uhumi wa nchi hiyo.