Muigizaji wa Bongo Movie, Salma Jabu maarufu kama Nisha amewachana wanaume wenye tabia za kupenda kulelewa, kuhudumiwa na wanawake.
Nisha amefunguka na kusema kuwa yeye binafsi ameshawahi kulea na kuhudumia wanaume wa dizaini hiyo.
Hata hivyo kwa sasa imekuwa tabia kwa wasanii wanawake wa bongo movie pamoja na wasanii wa muziki na wale waliopo kwenye urembo na mitindo kuwa na mahusiano na vijana walio na umri mdogo.
”Mimi ni miongoni mwa wanawake ambao nimekuwa na mahusiano na wanaume wanaopenda kutegemea kwa kila kitu”.
Amesema kuwa wanaume wenye tabia hiyo wengi hawapendi kufanya kazi kwa madai kuwa wanatunzwa na wanawake walionao kimapenzi.
Muigizaji huyo amesema kuwa mwanaume ambaye ni tegemezi hawezi kudumu naye na inafikia kipindi humkana kabisa mbele ya watu.
Amesema kuwa ” Siyo kwamba mtu hanauwezo wa kufanya kazi lakini anataka kupewa kila kitu mimi sitowezana naye na kama kuna mwanaume wa aina hiyo amekaa akisubiri nafasi hiyo kwangu amefeli”.
Pia amesema kuwa wapo wanawake wenye tabia ya kutegemea kila kitu kwa mwanaume wakati uwezo wa kujishughulisha upo, hivyo amewasihi watu kujishughulisha na kuachana na dhana ya kuwa mzigo kwa wenzi wao.