Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imekwama kutoa hukumu ya kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa sababu anaumwa.
Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ambapo Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro alieleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa mteja wake ameshindwa kufika Mahakamani kwa sababu anaumwa.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi August 30, mwaka huu kwa ajili ya hukumu.