Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Uhispania kwa ajili ya tuhuma za ukwepaji kodi nchini humo.
Ronaldo anatuhumiwa kukwepaji kodi mwaka 2010 wakati wa mauzo ya haki ya picha zake ndani ya nchi ya Uhispania.
Amepandishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za ukwepaji kodi wa euro milioni 14.7, nchini humo ambapo ni kosa kisheria.
Ronaldo amepata kosa hilo kama ilivyokuwa kwa mpinzani wake mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi.
Ronaldo anatarajia kuungana na klabu yake Real Madrid kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Manchester United Agosti 8 mwaka huu.
.