Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wataweka jiwe la msingi mradi wa bomba la kuasafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Bomba hilo litajengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ifikapo Agosti 5, 2017.

Taarifa hiyo imetolewa kutoka Ikulu ambapo imeeleza kuwa takribani ajira 10,000 zitazalishwa katika ujenzi wa mradi huo.

Watanzania watanufaika kwa kiasi kikubwa, hivyo watanzania wametakiwa kufuatilia uwekaji wa jiwe la msingi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *