Mtangazaji wa Clouds FM radio, Shaffih Dauda ametangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa shirikisho la soka nchini TFF.

Dauda alikuwa anagombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini TFF.

Shaffih Dauda ambaye ni mkuu wa vipindi wa Clouds FM amesema kuwa amefikia uamuzi huo wa kujitoa katika uchaguzi kutokana na siasa za mpira wa Tanzania.

Amesema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kuona mbinu na siasa chafu zinazoendelea dhidi yake baada ya kukamatwa na Takukuru akiwa mkoa Mwanza pamoja na baadhi wa viongozi wa chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam.

 Shaffih amesema kuwa alikwenda Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya ndondo cup mkoani humo lakini anashangaa amekamatwa na Takukuru.

Amesema kuwa hataki mambo yake binafsi ( kugombea uongozi TFF ) uharibu malengo ya Ndondo Cup na taasisi anayofanyia kazi.

Mwisho amesema kuwa amejitoa rasmi katika uchaguzi mkuu wa TFF na ataendelea kuchangia kwenye maendeleo ya soka nchi hii bila kuwa kiongozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *