Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amemuandikia barua rais mwenzake wa Guinea, Alpha Conde kumshukuru kwa maombi ya kitaifa aliyopanga ili kumwezesha kupona.

Buhari mwenye umri wa miaka 74 amekuwa nchini Uingereza kwa takriban siku 80 akipata matibabu kwa ugonjwa usiojulikana.

Katika barua yake ,bwana Buhari alimuhakikishia bwana Conde ambaye ndio mwenyekiti wa muungano wa Afrika kwamba alikuwa anaendelea kupona na kwamba atarudi nchini Nigeria ili kuendelea na huduma zake mara moja atakapoambiwa na daktari wake.

Katika barua ya mapema ,bwana Buhari alikuwa amekubali uteuzi wake kama kiongozi wa AU 2018 ajenda kuu ikiwa vita dhidi ya ufisadi.

Alichaguliwa kuchukua wadhfa huo katika mkutano wa AU mjini Ethiopia mnamo mwezi Julai 4.

Kutokuwepo kwa Bwana Buhari kumezua wasiwasi nchini Nigeria na kuzua uvumi kwamba wapinzani wake walikuwa wanapanga kumrithi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *