Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Julai 25, 2017 imeshindwa kuanza kusikiliza kesi kuhusu kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerard ‘Masogange’.
Kesi hiyo imehairishwa hadi Agosti 2, 2017 kutokana na wakili wa serikali kutokuwepo mahakamani kwa kuwa anauguliwa na mtoto .
Masogange anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kutumia dawa za kulevya aina ya Heroine na Oxazepam na Heroine (Diacety Imophine).
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).