Mwanamke mmoja amekamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Shenzhen nchini China akitokea Hong Kong na simu aina ya iPhone 102 akiwa amezifunga kiunoni tayari kwa kuziingiza nchini humo kiholela.
Mwanamke huyo aliyejifunga simu hizo kiunoni kwa kutumia tepu huku akiwa amevalia nguo nzito alishitukiwa na wahudumu wa uwanja huo wa ndege baada ya kubaini muonekano wake kutokuendana na viungo vingine kama mikono na miguu.
Wakaguzi hao wamesema walimkuta na simu na saa za mikononi ambapo kwa ujumla vilikuwa na uzito wa Kilogramu 19 .
Watu wengi wanafanya biashara hiyo kutokana na bei ya simu aina ya iPhone kuuzwa bei kubwa ukilinganisha na bei inayouzwa simu hizo, Hong Kong.
Serikali ya China ilitangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa zote za Kampuni ya Apple INC ili kuchochea mauzo ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.