Mwanamuziki nyota wa Marekani, Chris Brown amesema kuwa anajipanga kumshtaki promota kutoka Ufilipino, Jose Victor Los Banos kwa kujichukulia pesa kiasi cha dola 300,000 kwa njia ya utapeli.
Chris ameamua kufikia uamuzi huo baada ya kugundua kuna mipango ilipangwa kuchukua pesa hizo ambazo alizilipa miaka mitatu iliyopita.
Mwanamuziki huyo aliandaliwa shoo nchini Ufilipino katika Sikukuu ya Mwaka Mpya 2014 lakini hakutokea kwa sababu binafsi, badala yake aliomba kuirudia Julai 2015 ambapo-alipa-ngiwa ratiba na kuifanya ndani ya muda.
Baada ya kumaliza shoo hiyo akiwa hotelini akijiandaa kuondoka nchini humo alifuatwa na promota huyo na kumdai kiasi hicho cha pesa na kumwambia sababu ilikuwa kuingia mitini shoo ya kwanza ya 2014 na kuishinikiza idara ya uhamiaji kumzuia hadi atakapolipwa jambo lililotekelezwa.
Kwa sasa, Chris amefungua mashtaka hayo (haijatajwa mahakama) na kulalamika alipwe fidia.