Jaji Mkuu nchini Brazil ameagiza kushikiliwa kwa mali za Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Lula da Silva baada ya kukutwa na hatia ya rushwa.

Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Sergio Moro amesema kuwa kiasi cha dola za Marekani laki mbili zimegunduliwa katika akaunti ya kiongozi huyo wa zamani, hivyo kupelekea kushikiliwa kwa mali anazomiliki yakiwemo maghorofa matatu , ardhi kubwa ambayo alijimilikisha na magari mawili ya kifahari.

Rais wa zamani huyo wa zamani aliyejipatia umaarufu wa kuwatumikia wananchi wake kwa kuweka sera ya kuwajali wanyonge, alitumia fursa hiyo kuweza kujitajirisha kwa kuiba mali za umma.

Lula ataendelea kuzitumia mali zake hizo endapo atashinda katika rufaa yake aliyoikata ya kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama nchini humo ya kwenda jela miaka tisa na nusu iliyotokana tuhuma za rushwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *