Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kote nchini kutumia mashine stahiki za risiti za kielektroniki (EFDs).

Rais Magufuli amesea na kusisitiza kuwa watakaoshindwa kufanya hivyo watafutiwa leseni zao za biashara.

Hayo ameyasema leo mjini Biharamulo mkoani Kagera wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga.

Hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Prof. Philip  Mpango alivifungia baadhi ya vituo vya mafuta hapa nchini baada ya kubainika kuwa vilikuwa havitumii mashine stahiki za EFDs kinyume cha sheria jambo ambalo linaifanya serikali kukosa mapato yake kulingana na mauzo ya mafuta hayo.

Mpaka kufikia jana jumla ya vituo 710 vya mafuta vimefungwa na mamlaka ya mapato nchini (TRA) kutokana na kutotumia mashine za EFD’s.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *