Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye alijiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.
Akithibitisha kifo hicho, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa “ Mgonjwa amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’.