Klabu ya Chelsea wamedhamiria kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero mwenye umri wa miaka 29.
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic hayuko tayari kulipa fedha nyingi kumsajili Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo anaelekea Italia.
Chelsea wanataka kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang.
Dau la pauni milioni 2.6 la Manchester City kumtaka kipa wa Napoli, Pepe Reina, 34, limekataliwa.
Manchester City hawatakabiliwa na ushindani tena kutoka Bayern Munich katika kumsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka Arsenal baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge kusema hawamfuatilii tena.
Paris Saint-Germain wameingia katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis sanchez, 28.
Paris Saint-Germain wapo tayari “kuvunja benki” kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Neymar, na watakuwa tayari hata kulipa euro milioni 222, kulazimisha uhamisho wake.
Washauri wa karibu wa Neymar wanamshauri aondoke Barcelona ili kuepuka kufunikwa na Lionel Messi. Manchester City, PSG na Manchester United zote zinamtaka mshambuliaji huyo kutoka Brazil.
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona amesema hakuna timu itakuwa tayari kutoa pauni milioni 195 kumsajili Neymar, 25.
Manchester United wanafikiria kupanda dau la mwisho la pauni milioni 60 kumtaka kiungo wa Tottenham, Eric Dier, 23.
Zlatan Ibrahimovic, 35, ameonesha dalili kuwa atabakia Old Trafford baada na kuwaandikisha watoto wake katika akademi ya Manchester United.
Manchester United wanamtaka kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huku klabu yake RB Leipzig ikipunguza vikwazo. Mbali na United na Liverpool, pia Arsenal, Manchester City, Juventus na Inter Milan zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea.
Manchester United wana uhakika wa kukamilisha usajili wa Ivan Perisic katika saa 48 zijazo. baada ya kukubaliana na Inter Milan.
West Brom wanamtaka beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, lakini timu hizo mbili hazijafikia makubaliano yoyote.
Arsenal watajaribu kupunguza idadi kubwa ya wachezaji wake wasiotumika, kabla ya kufanya uamuzi wa kuvunja rekodi tena ya usajili na kumchukua Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco.
Monaco wamewaambia Arsenal watalazimika kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa takriban pauni milioni 80 kumsajili kiungo Thomas Lemar, 21.
Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 6.2 kutoka Sampdoria la kutaka kumsajili kiungo Jack Wilshere, 25. Arsenal wanataka pauni milioni 8.8.
Juventus wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumsajili Nemanja Matic, 28, au Steven N’Zonzi, au William Carvalho.
Inter Milan wanapanga kuwajaribu Real Madrid kwa kutoa dau kubwa kumtaka kiungo Toni Kroos.