Mapacha walioungana, Maria na Consolata wamejawa na furaha baada ya kufaulu mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita, katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa.

Maria na Consolata, walio na umri wa miaka 19, wamefaulu kwa kupata daraja la pili katika masomo yao ya kidato cha sita na kuwa na matumaini kuwa ndoto yao ya kuwa walimu hapo baadaye inaelekea kutimia.

Wanafunzi hao wamesema kuwa wangependa kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Ruaha mkoani humo.

Wameeleza sababu za kuchagua chuo kwenye mkoa wanaoishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao wangependa kubadili mazingira.

“Kwanza tunapenda mazingira ya Iringa, hatukutaka kwenda Dar es Salaam kwa sababu ya kwanza tunapenda kuishi pamoja na walezi wetu Masista waliokuwa wanatulea tukiwa wadogo na pili mikoa mingine ni mbali na tunapoishi. Pia ni kwa sababu kwa hali yetu tulivyo hatumudu kuishi kwenye mazingira ya joto.

Maria na Consolata wanaona kuwa, hakuna linaloshindikana iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *