Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imesogeza mbele zoezi la ulipaji kodi ya majengo hadi ifikapo Julai 31 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona bado kuna watu wengi wanahitaji kulipia kodi hiyo.
Alisema kwaJiji la Dar es Salaam zimetengwa ofisi maalumu kwa ajili ya kazi hiyo hiyo ili kutoa fursa kwa ofisi nyingine kuendelea kukusanya kodi nyingine.
Ofisi zitakazoendelea na zoezi hilo kwa Dar es Salaam ni TRA Mbagala, Temeke, Kigamboni, Kimara, Tegeta, Manzese, Ilala, Gerezani, Vingunguti, Samora, Kijitonyama na ofisi ya TRA ndani ya viwanja vya Sabasaba.
Kayombo amesema baada ya Julai 31 watakaolipa kodi hiyo wataambatanisha na faini.