Mke wa Said Mrisho aliyetobolewa macho na Salum Njwete ‘Scorpion’ amefunguka makubwa kuhusu kutelekezwa na mumewe huyo licha ya kuwa na matatizo ya macho.
Mke huyo wa Said Mrisho aliyejitambulisha kwa jina, Stara Sudi amsema tukio hilo limetokea hivi karibuni siku chache baada ya wawili hao kuhamia kwenye nyumba ya kupanga maeneo ya Majichumvi jijini Dar es Salaam.
Yafuatayo ni maenelezo ya mwanamke huyo anayedai kutekelezwa na Said Mrisho aliyetobolewa macho na Scorpion.
“Baada ya kuhamia Majichumvi, siku hiyohiyo Said akaniambia anatarajia kusafiri usiku, hivyo nimuandalie nguo na mimi bila kusita wala kuwa na wasiwasi nilifanya kama alivyoniagiza, akaja akachukua nguo na kusema tena atalala kwa rafiki yake ili wadamke usiku, akaondoka lakini baadaye alinipigia simu na kuniuliza kama nilikuwa bado naweka vitu sawa na kunijulisha kuwa kuna mahali amekaa akipata chakula.
“Alipomaliza kuniambia hivyo, akadhani simu imekatika lakini bado ilikuwa hewani akawa anasema yaani huyu anadhani ninasafiri, nitamkimbia taratibu hadi tuachane kabisa, hakika niliumia na kuanza kulia kujua kumbe mume wangu ananifanyia uhuni wakati nina watoto wanne wengine wakiwa wachanga wa mwezi mmoja,” alisema Stara na kumalizia;
“Kuna nyumba ya zamani ambayo tulitaka kuhamia kabla ya huku Majichumvi na kuna baadhi nya vitu vyetu vilikuwa huko, nikampigia simu mama na hapohapo mimi na dada yangu tukaenda huko kubahatisha kama tutamkuta, kweli tulimkuta na alianza kufanya fujo akampiga mtoto na dada yangu, baadaye kesi ikahamia polisi, akiwa amenisingizia kwamba mimi na ndugu zangu tumemfanyia fujo na kumuibia shilingi milioni mbili, tukashauriana suala hilo lifike Ustawi wa Jamii ambapo kesho tutafanya hivyo,” alisema Stara.