Mwanamuziki wa nyimbo za reggae nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine ameapishwa leo kuwa mbunge wa Kyadondo East nchini Uganda.

Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 29 mwezi Juni.

Alisema kuwa anaingia bungeni kama kiongozi na wala si mwanasiasa, kwa mujibu wa gazeti la New Vision.

Chama tawala NRM na upinzani wamekuwa wakimtaka Wine ajiunga na mmoja wao ili kuviimalisha vyama vyao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *