Simba wanne wametoroka katika mbuga ya taifa nchini Afrika Kusini na hawajulikani walipo.

Simba hao walitoroka kutoka mbuga ya Kruger siku ya Jumapili na mara ya mwisho walionekana katika kijiji cha Matsulu.

Usimamizi wa mbuga hiyo sasa umewataka wenyeji kuchukua tahadhari

Haijabainika vile simba hao walifanikiwa kutoroka kutoka mbuga hiyo inayozungukwa na ua.

Mbuga ya kitaifa ya Kruger ni moja ya mbuga kubwa zaidi barani Afrika ikiwa na ukubwa wa kilomita 19.485 mraba.

Kisa hiki kinatokea baada ya simba wengine watano kutoroka mbuga hiyo mwezi Mei. Wanne walipatikana lakini mmoja bado hajulikani aliko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *