Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana baada ya kukaa rumande kwa siku sita kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.
Mdee ameachiwa leo kwa dhamana ya milioni 10 na wadhamini wawili baada ya kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu na hakimu mkazi mkuu Victoria Nongwa.
Wakili wa Serikali Nassoro Kasuga amedai kuwa Mdee akiwa makao makuu ya Chadema alitoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli.
Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika lakini mbunge huyo kwasasa yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi vigezo vya kupata dhamana.