Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe leo amesitisha uteuzi wa mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Waziri Mwakyembe amesema kuwa kuanzia leo kutokana na mamlaka mamlaka aliyopewa na sheria ya BMT Na.12 ya 1967 amesitisha uteuzi huo.

Kusitisha kwa uteuzi huo kunatokana na agizo alilopewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyemwagiza afanyie kazi mapitio na kulitathmini upya baraza hilo ili kujiridhisha na usimamizi wake kuhusu michezo.

 Kutokana na kujiridhisha kwake kwamba usimamizi wa BMT si imara, amelivunja na ataliunda upya.

Kwa sasa sekretarieti ya baraza hilo itaendelea kufanya kazi katika kipindi hiki ikishirikiana na wizara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *