Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wamemtaka Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kujiuzuru kutokana na umri wake.
Wapinzani hao wamemlaumu Mugabe kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kuenda Singapore kwa matibabu.
Gazeti la kibinfasi la News Zimbabwe lilimnukuu Obart Gutu, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC.
“yeye bado si kijana mdogo, njia hii anajiadhibu sio nzuri kwa afya yake ya kimwili na kiakili.
Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya.”
Karauone Chihwayi, msemaji wa upande uliojitoa MDC naye alitoa matamshi kama hayo.
“Nchi hii imekwama leo hii kwa sababu rais wa Zanu anaongoza akiwa kitanda cha hospitali.”
Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.