Klabu ya Everton wametoa dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27.

Baada ya kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton, Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, baada ya kukubaliana mkataba wa pauni milioni 35. Chelsea wanamtaka pia Bakayoko (Daily Star).

Arsenal wapo tayari kupanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 45 kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar, baada ya dau la pauni milioni 30 na 40 kukataliwa (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 28, amedhamiria kupigania nafasi yake Emirates, licha ya kuhusishwa na kuhamia West Ham kwa pauni milioni 20 (Daily Star).

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kuimarisha eneo la kiungo kwa kumsajili Marcelo Brozovic kutoka Inter Milan (ESPN).

Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 27, ambaye amehusishwa na kuhamia Juventus, ameachwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Australia kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya (Sun).

Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata baada ya kumkosa Romelu Lukaku (AS).

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumsajili beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19 kwa pauni milioni 10 (Daily Mirror).

Real Madrid wapo tayari kumuuza kiungo Mateo Kovacic, na Tottenham wamehusishwa na kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia (Evening Standard).

Cristiano Ronaldo atabakia Real Madrid msimu wa 2017-18 na hivyo kufuta uvumi wa kuhamia Manchester United (AS).

Newcastle wanajaribu kukamilisha usajili wa kiungo wa Norwich Jacob Murphy, 22, kwa pauni milioni 8.5, huku Southampton na Crystal Palace wakimtaka pia mchezaji huyo (Daily Mirror).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *