Rais wa Marekani, Donald Trump na rais wa Uturuki, Vladimir Putin wamekutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza kabisa, na wakasalimiana kwa mikono kwenye mkutano wa G20 mjini Hamburg, Ujerumani.

Viongozi hao wa Marekani na Urusi wamesema wanataka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao uliathiriwa na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.

Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara yanatarajiwa kutawala mazungumzo katika mkutano huo mkuu wa siku mbili.

Mke wa rais wa Marekani Melania Trump ameshindwa kuondoka katika hoteli ambapo amekuwa akikaa katika jiji hilo la Ujerumani kutokana na maandamano.

Alikuwa amepangiwa kufanya matembezi mafupi pamoja na wake wengine wa marais wanaohudhuria mkutano huo.

Mkutano wa G20 (Kundi la mataifa Ishirini) huwa ni mkutano wa nchi 19, zilizostawi na zinazostawi, pamoja na Umoja wa Ulaya (EU).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *