Golikipa wa Arsenal, Petr Cech amesema kwamba anatarajia kocha wake Arsene Wenger atasajili wachezaji sahihi kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hiko na kutwaa taji kwa mara ya kwanza toka mwaka 2004.
Wenger hadi sasa amesajili wachezaji watatu kwenye kikosi hicho baada ya kuwanunua kiungo, Granit Xhaka, beki Rob Holding na mshambuliaji Takuma Asano.
Petr Cech amesema kwamba ni lazima kununua wachezaji unaowahitaji kwenye kikosi chako ili kuimarisha timu na siyo kununua tu wachezaji wasiofaa ni kupoteza ela.
Arsenal ilikuwa inataka kumsajili mshambuliaji wa Leicester, Jamie Vardy lakini walimkosa baada ya kuongeza mkataba na mabingwa hao wa ligi kuu nchini Uingereza na vile vile ofa yao ya paundi milioni 38 imekataliwa na Olimpique Lyon kwa ajili ya kumsajili Alexandre Lacazette.
Klabu hiyo ya Arsenal itaanza mechi yao ya kwanza kwenye ligi kuu nchini Uingereza watakapo waalika Liverpool katika uwanja wa Emarates Agosti 14 mwaka huu.