Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelaani kitendo cha wabunge 8 wa upinzani kukamatwa na jeshi la polisi kwa madai yakutaka kumpiga mbunge wa CCM Juliana Shonza.
Freeman Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni aliyasema hayo jana Dodoma baada ya kutoka mahakamani na kudai kuwa wao wanaamini kuwa mahakama itatenda haki kwa wabunge hao.
Pia Mbowe amesema kitendo cha Spika wa Bunge, Job Ndugai kulivalia njuga suala hilo ni jambo ambalo yeye limemsikitisha sana kama kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni.
Mbowe amesema kuwa “Kitendo cha kuwapeleka polisi na kuwashtaki wabunge wetu na Spika wa Bunge kushadadia jambo hili limenisikitisha sana
Katika watuhumiwa wote nane, mtuhumiwa mmoja ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mbunge Saed Kubenea jana alipandishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa moja la shambulio la kawaida hivyo alidhaminiwa na shauri hilo upelelezi wake bado haujakamilika hivyo kesi itatajwa tena tarehe 26, Julai 2017 Dodoma.