Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema siku za wahalifu wanaofanya uhalifu wilayani Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani zinahesabika.

IGP Sirro amesema hayo  jana  alipokuwa katika ukumbi wa Police Officer’s Mess, Oysterbay Dar es Salaam wakati akikabidhiwa magari manne na kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval na kudai kuwa magari hayo yatasaidia kupambana na uhalifu  nchini.

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval alisema msaada huo wa magari ambao wameutoa kwa jeshi la polisi nchini ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa za jeshi hilo katika kupambana na uhalifu nchini.

Mpaka sasa ni zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha mkoani Pwani kwa kuuliwa na watu wasiojulikana huku wengine kadhaa wakiwa wamejuruhiwa kwa risasi na watu hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *