Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji amesema anataka kutumia bajeti ya Sh. Bilioni 5.5 kwa msimu kwa ajili ya Simba SC, ili kuwapiku wapinzani Azam na Yanga kama akipewa timu hiyo.
Dewji amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa Habari, ofisini kwake, jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
Mohamed Dewji ambaye ni mbunge wa zamani wa Singida amesema atayafanya hayo iwapo Simba SC watakubali kumuuzia asilimia 51 ya hisa kwa Sh.Bilioni 20.
Vile vile ameongeza kwa kusema akiuziwa asilimia 51 ya hisa na kuwa mmiliki wa Simba, atawawezesha wanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo kupewa hisa bure, ambazo wataamua wenyewe kuuza, au kununua hisa zaidi.
Mwenyekiti huyo wa Kapuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) amesema shabaha yake ni kuitoa klabu kwenye bajeti ya bilioni 1.2 hadi bilioni 5.5 na mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, lazima wasajili vizuri, waajiri kocha mzuri.
Mohamed Dewji ni mpenzi na mshabiki wa klabu ya Simba SC ambapo anahitaji timu hiyo kwa ajili ya kununua hisa ili aitoe hapa iliyopo na kuipeleka mbali zaidi lakini juhudi zake zinaonekana kugonga ukuta baada ya wanachama wa klabu hiyo kugoma kumuuzia hisa hizo.