Klabu ya Everton imekamilisha usajili wa beki wa kati Michael Keane kutoka Burnley kwa ada ya pauni milioni 30.

Keane amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea klabu hiyo na unakua usajili wa tano kwa Everton katika majira kiangazi.

Everton tayari imewasajili golikipa Jordan Pickford, kiungo Davy Klaasen, mshambuliaji Sandro Ramirez pamoja na Henry Onyekuru.

The toffes imekwisha tumia kiasi cha pauni milioni 96 katika usajili wa nyota hao wapya .

Klabu ya zamani ya Michael Keane, Man United itapata mgawo wa kiasi cha pauni milioni 7.5 katika usajili huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *