Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza kamanda wa polisi wilaya ya Kinondoni, Suzan Kaganda kumkamata na kumuweka ndani masaa 48 mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli.
Mdee anadaiwa kutoa maneno hayo ya kukashifu na uchochezi katika mkutano wake wa Baraza la wanawake Chadema (Bawacha) uliofanyika jana katika makao makuu ya chama hicho.
DC Hapi amesema kuwa kauli za Mdee kuhusu wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni imemshtua yeye kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wiliya huyo amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari ofisi kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pia amesema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo hasa baada ya Mdee kumshushia kashfa hizo kiongozi wa nchi ambaye ni amri jeshi mkuu.