Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amepinga muswada wa mabadiliko ya sheria ya maliasili, wakati akichangia hoja huku akiwatuhumu wabunge wa CCM kufanya mambo kwa ushabiki.
Lema amesema sheria zilizoligharimu taifa mpaka sasa, zilipitishwa kishabiki bungeni, kama ambavyo wabunge wanataka kufanya hivyo sasa hivyo kama ushabiki utaendelea, lazima sheria zitakazopitishwa zitakuwa ni zilezile.
Kutokana na kauli hiyo ya Lema, Waziri TAMISEMI, George Simbachawene amemkosoa Lema kwamba alikuwa akikiuka sheria katika uchangiaji wake.
Baada ya Simbachawene kukaa chini, Lema alimpiga kijembe kwamba anataka kubadilishiwa wizara ndiyo maana anapinga hoja ya Lema.
Akataka utengwe muda wa kutosha kujadili muswada huo na si kupeleka bungeni kwa hati ya dharura.
Mjadala mkali uliendelea ambapo Lema aliendelea kutoa hoja nzito akizielekeza upande wa wabunge wa CCM.