Qatar imepewa masaa 48 kutimiza masharti 13 iliyopewa na nchi za Kiarabu ikiwemo kukifunga kituo chake cha habari cha Alja Zeera vinginevyo itaongezewa masharti mengine ambayo yataisababishia matatizo makubwa ya mahusiano na nchi hizo.

Majibu hayo yatazingatia masharti 13 yaliyotolewa baadhi yakiwa ni kufunga televisheni ya Al Jazeera, kufunga kambi ya kijeshi ya Uturuki jijini hapa, kusitisha ufadhili kwa vikundi vya kigagidi na vyenye msimamo mkali, na kupunguza uhusiano wake na Iran.

Qatar iliwekewa masharti hayo na mataifa sita yakiongozwa na Saudi Arabia. Mataifa mengine matatu ya Kiarabu yaliwakilisha masharti 13 kwa Qatar kama milango ya kutatua mzozo unaoikumba ghuba hiyo.

Mataifa mengi ya ghuba yalitangaza kusitisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar kwa madai taifa hilo linajihusisha kuunga mkono makundi ya kigaidi, jambo ambalo Doha imekanusha na kutaka nchi hizo kutoa ushahidi wa kutosha.

Mbali ya kuvunja uhusiano wa kidiplomasia, pia zilifunga mipaka na usafiri wa anga, bahari na ardhi.

Tarehe ya mwisho iliyowekwa na mataifa hayo kwa Qatar kutoa jibu ilikuwa jana Julai 2, lakini  iliongezewa  masaa 48.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *