Michuano ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa (Confederation Cup) inatarajiwa kuhitimishwa leo pale ambapo timu ya taifa ya Ujerumani itakapo cheza dhidi ya Chile hatua ya fainali.

Katika hatua ya makundi timu hizo zimeshakutana na kushindwa kuamua mbabebaada ya kila timu kuchomoza na ushindi wa goli moja moja.

Timu ya taifa ya Chile na Ujerumani zitakutana tena katika hatua ya fainali ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa (Confederation Cup) Jumapili hii.

Chile wametinga katika hatua hiyo ya fainali usiku wa Jumatano kwa mara ya kwanza baada ya kuinyuka Ureno kwa mikwaju ya penati 3-0 baada ya kutoka sare ya kutofungana katika dakika 120 za mchezo huo.

Wakati Ujerumani was njia ya kutinga hatua ya fainali ikionekana nyepesi baada ya kuchomoza na ushindi mono wa magoli 4 -1 dhidi ya Mexico.

Mchezaji Leon Goretzka alikuwa mwiba mkali ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kuifungia timu yake magoli mawili ya mapema yaliyochangia kuivusha hatua ya nusu fainali.

Mexico itacheza na timu ya taifa ya Ureno latina kuwania nafasi ya tatu ya michuano hiyo, ambapo mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo hatakuwepo katika mchezo huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *