Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnum jana amezindua bidhaa yake ya karanga zitakazojulikana kwa jina la ‘Diamond Karanga’ ambazo zikipatikana nchi nzima.

Diamond amezindua bidhaa hiyo jana katika Viwanja vya Karume Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuitambulisha kwa mashabiki wake na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Diamond amedai lengo lake kubwa ni kusaidia kutoa ajira kwa vijana ambao wanatatizo la ukosefu wa ajira nchi.

Diamond amedai yeye ni mfanyabishara kwa hiyo amekuwa akiangalia njia mbalimbali za kufanya biashara ambazo itamwingizia pesa kupitia brand yake pamoja na kuwanufaisha watu wengine.

Amesema kuwa “Kwa hiyo wanangu wote ambao tunauza Karanga, wataacha kuuza zile zamkononi na kuanza kuuza bidhaa ambayo imefungwa vizuri kwenye mifuko kwa bei nzuri lakini pia mtu ambaye anataka kuzinunua akizuangalia atavutiwa nazo”.

Baada ya uzinduzi wa bidhaa hiyo Diamond sasa anakuwa anamiliki bidhaa mbili ambapo hapo awali tayari amezidua bidhaa ya Perfume “Chibu Perfume’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *