Mkali wa hip hop kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka kwa kusema kuwa kampuni yao kwa sasa haina ushamba tena kwenye muziki kwa kuamini kuwa video ndiyo inaweza kukuza muziki wao na kuwapeleka sehemu kubwa zaidi.

Joh Makini, amesema kuwa anacho amini kwenye muziki ni ladha ya muziki mzuri ‘audio’ ndiyo inaweza kuuza muziki huo japokuwa ni vizuri muziki ukiwa na video.

Amesema kuwa “Mimi naamini kitu cha kwanza kwenye muziki ni audio, Ndiyo maana unaona watu zamani tulikuwa tunapiga audio strong na ilikuwa inauza…, Watanzania wameshaacha ushamba wa picha ndio maana hata ukitoa video kali kama audio sio nzuri ngoma inakufa”.

Katika hatua nyingine Joh Makini amefunguka kuhusu suala la mashabiki kutumiana nyimbo kupitia mitandao na kwamba  watumie njia sahihi  ili kusapoti kazi za wasanii wanaowakubali.

Pia amesema kuwa “Watu waache kutumiana audio kwenye Whats App au makundi halafu kwenye interview unakuta mtu anaulizwa album lini, kama umeshindwa kununua ngoma moja mtandaoni utawezaje kununua album?”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *