Mwandishi mahiri wa mfululizo wa hadithi za Harry Potter, J.K. Rowling ameikemea tovuti inayotumia jina na picha yake kutangaza semina ya uandishi wa vitabu.

“Ninachukia mambo ya aina hii na sipendi picha yangu itumike kuitangaza semina hii’ ameandika Rowling kwenye akaunti yake ya Twitter.

‘Msipoteze pesa zenu’ Akamalizia.

Kwenye meseji hiyo ya Twitter, mwandishi huyo amejumuisha link ya website inayodai kuandaa semina ‘baab kubwa ya uandishi wa habari utakaowafanya watakaohudhuria kuwa mabilionea kama Rowling.

Shirika la utangazaji la Marekani la CNN lilijaribu kuwasiliana na tovuti hiyo ya ‘bestsellerent.com’ bila mafanikio.

Mtu anayetangaza semina hiyo aambaye amejitambulisha kwenye tovuti hiyo kwa jina la Darren Stephens amekuwa akiuza nafasi ya ushiriki wa semina hiyo ya siku tatu kwa $4,997 (10m) kwa kila mshiriki.

Semina hiyo imepewa jina la “how to write a best seller and create your 6-7 figure empire.”

Kwa sasa tovuti hiyo inauza nafasi za ushiriki wa semina hiyo kwa ‘ofa chache maalum’ kwa $97 (laki 2).

Tovuti hiyo inatumia majina ya watu wengi maarufu mbali ya Rowling kwaajili ya kuuza semina hiyo ambapo majina mengine yanayotumika ni pamoja na rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton na mgombea urais wa Marekani Donald Trump.

Tovuti hiyo imedai kuwa semina hiyo itafanyika baina ya 26, 27 na 28 Agosti nchini Australia.

Stephens anayetajwa kama CEO (bila kutajwa kampuni yake) na ametajwa kwenye tovuti hiyo kuwa mwandishi aliyefanikiwa kuuza nakala nyingi za vitabu lakini majina ya vitabu alivyoandika hayajaorodheshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *