Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa leo ameripoti kwa mara ya pili makao makuu ya jeshi la Polisi nchini.

Lowassa amewasili leo makao makuu hapo akiwa na viongozi wengine wa Chadema akiwemo, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambapo ulinzi uliimarisha katika eneo hilo.

Lowassa alitakiwa kuwasili leo makao makuu hayo kutokana na kutoa kauli za uchochezi wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara Juni 23 mwaka huu.

Lowassa ambaye ni waziri mkuu mstaafu anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Zanzibar wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa na magereza akidai kuwa sheria ifanyike ili kuwaachia huru masheikh hao.

Akiongea katika viunga vya makao makuu hayo, Mbowe amesema kuwa Lowassa anatarajiwa kurudi tena makao makuu hayo Julai 13 mwaka huu kutokana na upelelezi bado ujakamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *