Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, Katibu wake Celestine Mwesigwa pamoja na Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ wafikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazowakabili.
Viongozi hao jana walipelekwa Polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yao kwa tuhuma za rushwa zinazowakabili.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walipelekwa walipelekwa Makao Makuu ya Takukuru kwa ajili ya uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.