Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amempongeza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kwa kuzuia maroli zaidi ya 100 yaliyokuwa yanasafirisha mahindi nje ya nchi.

Waziri mkuu alipiga marufuku usafirishaji wa mahindi alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya Eid El Fitr.

Baada ya agizi hilo maroli yalikamatwa na kuzuiwa mara moja kutosafirisha mahindi nje nchi na badala yake wauze mahindi hayo ndani ya nchi.

Akijibu maswali ya papo kwa papo Bungeni leo, Waziri Mkuu amesema kuwa uhamuzi huo ni moja ya hatua za kuhakikisha taifa linajihadhari na ukosefu wa chakula.

Waziri mkuu amesema kuwa anampongeza mkuu wa mkoa huyo na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa kuzuia maroli hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *