Mji mkuu wa Angola uitwao Luanda umeshika nafasi ya kwanza kama mji ghali zaidi duniani kuishi na nafasi ya pili kushika Hong Kong.

Hii imetokana na takwimu za gharama ya kuishi kutoka na utafiti ulifanywa na shirika la Mercer

Miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi tano za kwanza duniani kwa kuwa na gharama ya kuishi.

Mji wa London ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya pauni ambayo ndiyo ela ya nchi hiyo.

Utafiti huo wa kila mwaka huangazia masuala kadha kando na gharama ya kukodi nyumba ndani ya miji.

Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *