Muigizaji wa Bongo Movie na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi amewashauri vijana wanaotaka kuingia katika tasnia ya sanaa kuepuka vishawishi vya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Snura amebainisha hayo baada ya kutuhumiwa akijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinamfanya kumpa mizuka ya kufanya vizuri pindi akiwa stejini akitumbuiza.

Snura amesema kuwa “Vijana wenzangu kama mnaingia kwenye sanaa achaneni na vishawishi, kuna vishawishi vya kipumbavu sana, eti uonekane unaenda na wakati na ndiyo vinawaponza watu wanaingia kwenye dawa za kulevya.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Mimi napanda kwenye steji situmii kilevi cha aina yeyote Mungu wangu aliyekuwa mbinguni ni shahidi sinywi pombe sivuti na nina panda kwenye steji nafanya vizuri tu kiasi kwamba wewe unaweza kufikiri nimetumia kilevi kwa sababu akili yangu nimeijenga kwamba hii ni kazi”.

Muigizaji huyo ambaye pia ni muimbaji amewataka wasanii hao kuwa makini kutokana na majanga hayo ya matumizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *