Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anatuhumiwa kwa kosa la kukwepa kodi wakati alipokuwa katika klabu ya Real Madrid nchini Uhispania.
Maafisa wa mashtaka nchini humo wanasema alitenda makosa hayo alipokuwa mkufunzi mkuu wa klabu hiyo.
Anatuhumiwa kukwepa kolipa kodi ya jumla ya €3.3m (£2.9m; $3.6m) kati ya mwaka 2011 na mwaka 2012.
Watu wengine mashuhuri aktika soka ambao wametuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa kulipa kodi Uhispania majuzi ni pamoja na nyota wa Barcelona Lionel Messi, ambaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela.