Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa hawezi kuchukua fomu za kugombea urais wa TFF kutokana na kuwa na majukumu mengi.

Zitto Kabwe amedai kuwa atashindwa kuzitumikia kofia tatu kwa wakati mmoja na badala yake ameamua kuachana na nafasi hiyo.

Zitto amebainisha hayo baada ya kupokea maombi kwa baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wakubwa wakimtaka akachukue fomu ya Urais TFF pindi dirisha likifunguliwa ili aweze kugombea nafasi hiyo hapo awali.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Facebook amesema kuwa “Nimetafakari na kuchukua uamuzi kwamba uongozi wa ACT- Wazalendo na Ubunge ni nafasi ambazo ninazo tayari, wakati Urais TFF ni nafasi mpya. Kwa hali hiyo na kwa mapenzi makubwa ya soka la Tanzania, nimeamua nisichukue fomu ya kugombea Urais TFF kwani naweza kuomba kazi ambayo nitashindwa kuitumikia kwa muda wa kutosha kutokana na majukumu yangu kwenye chama na Ubunge”.

 Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo na mbunge Kigoma Mjini ameendelea kwa kusema uamuzi wake umezingatia umezingatia mapenzi makubwa ya kwa soka la Tanzania.

Mwisho amemaliza kwa kusema kuwa ” Nikijitokeza kuwania Urais wa TFF leo halafu nikakosa muda mzuri wa kutimiza matarajio ya wapenda soka nchini, utakuwa ni usaliti mkubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *