Kundi la wananchi zaidi ya 400 kutoka baadhi ya kata zinazopakana na mgodi wa dhahabu wa North Mara wilayani Tarime mkoani Mara wanaotakiwa kuhama kupisha shughuli za uchimbaji, wamevamia mgodi huo jana wakidai malipo ya fidia.

Wananchi hao ambao maeneo yao yalifanyiwa tathmini tangu mwaka 2014 bila kulipwa hadi sasa, wanadaiwa kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha iliyotoka hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Andrew Sata amethibitisha kutokea kwa jaribio la kuvamia mgodi uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Kamanda huyo amesema kuwa hakuwa mtu yoyote anayeshikiliwa na jeshi la polisi kuhusu uvamizi wa mgodi huo siku ya jana.

Tukio hilo limetokea jana kwenye mgodi huo huku kukisadikiwa baadhi ya wananchi waliondoka na madini ya dhahabu wakati wa uvamizi huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *