Timu ya taifa ya Chile imeibamiza Cameroon 2-0 kwenye mechi ya kombe la mabara iliyofanyika jana nchini Urusi.
Goli la kwanza la Chile lilifungwa na kiungo anayekipiga klabu ya Bayern Munich, Arturo Vidal katika dakika ya 82 huku goli la pili likifungwa dakika ya 90 na Eduardo Vargas.
Cameroon wameonekana kucheza kwa kujiami sana kwa kulinda zaidi na kushambulia kwa kushtukiza kwenye mechi hiyo.
Katika kundi A timu ya taifa ya Ureno walitoshana nguvu na Mexico kwa sare ya mabao 2-2, Ricardo Quaresma alianza kuipatia Ureno goli la kuongoza katika dakika ya 35
Mexico walisawazisha goli hilo kupita kwa Javier Hernandez Chicharito na kumfanya mshambuliaji huyu kuwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa akifikisha mabao 48.
Beki Cedric Soares akaongeza bao la pili kwa Ureno katika dakika ya 86 kabla ya Hector Moreno kusawazisha goli hilo kwa upande wa Mexico katika dakika za lala salama.